Panya road waua, wadhibitiwa Dar

DAR ES SALAAM-Vibaka waliojaribu kutishia amani wakazi wa Vingunguti na maeneo jirani ya Tabata, Ilala, Dar es Salaam walidhibitiwa na Jeshi la Polisi.

Vibaka hao walikusudia kushambulia raia kwa silaha za jadi, mapanga na visu kwa lengo la kulipiza kisasi baada ya kibaka mwenzao kuuawa na wananchi wenye hasira baada ya kumpora simu dada mmoja eneo la Guest House.

Baada ya mazishi ya kibaka huyo yaliyofanyika Julai 31, 2023 jioni katika makaburi ya Vingunguti, Kichangachui, vibaka hao walitawanyika mtaani na kuanza kushambulia na kujeruhi watu kwa visu.

Wakazi wa Vingunguti, saa 10:00 tu za jioni, tayari walikuwa wameingia kulala, wafanyabiashara, Biashara zao na maduka wakafunga.

Wanaume wawili, Masau Kuliga Bwire (Mzalendo) na Chande Msoka (M/Kiti Mtaa wa Majengo), tulibaki tukizunguka mtaani kuwasaka vibaka hao, mtaa ulikuwa kimya, watu wote wamefunga majumba yao wamelala.

Tuliwasiliana na Jeshi la polisi ambao walifika na Defender nne kuimarisha ulinzi, wakiongozwa na Kamanda wa Kanda maalumu (Jumanne Mriro), OCD Buguruni (Kyaruzi), OC-CID Buguruni (Simba).

Hata hivyo, kabla ya Jeshi la polisi kufika, vibaka hao walikuwa tayari wamejeruhi watu kadhaa, kati yao, watu wawili wamepoteza maisha akiwemo mjamzito Khadija ambao walichomwa visu.

Khadija, mkazi wa Ubungo, ambaye alikuwa akifanya biashara ya kuuza duka la dawa za binadamu Vingunguti, Koloni, alifunga duka mapema kukimbia vurugu za vibaka hao, akiwa stand ya daladala, barabara ya Machinjioni-Barakuda, njia panda ya Koloni, alivamiwa na vibaka hao wakamchoma visu kadhaa mwilini.

Alijikokota hadi nyumba ya jirani kujiokoa, akitokwa na damu nyingi, baadaye alikimbizwa Kituo cha Afya Plan, ambapo alipoteza maisha.

Kwa sasa hali imetulia, maana usiku kucha askari polisi wamekesha wakifanya Doria. Vibaka kadhaa wamekamatwa na watu kadhaa waliojeruhiwa wamelazwa Hospitalini, akiwemo muhudumu wa guest house ya Mashina Christina aliyechomwa visu vinne, amelazwa Hospitali ya Rufaa Amana.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news