Pima afya kabla ya mazoezi-Prof.Janabi

DODOMA-Mkurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof.Mohamed Y. Janabi amewataka wananchi kupima afya zao kabla ya kufanya mazoezi ili kusaidia katika kuboresha afya na kinga ya mwili.

Prof. Janab ameyasema hayo Agosti 10,2023 jijini Dodoma wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusu taarifa utekelezaji wa shughuli mbalimbali na mwelekeo wa mwaka wa fedha 2023/24

Aidha, Prof. Janabi amesema kuwa, kupima afya kunasaidia kujua uwezo wa mwili katika kukabiliana na mazoezi ambayo hufanywa kama vile mpira na kukimbia.

Hata hivyo, Prof.Janabi amesema kuwa, katika kukabiliana na maradhi mbalimbali ikiwemo tatizo la moyo ni vyema kwa wananchi kupima mara kwa mara afya zao kwani baadhi ya magonjwa ni ya ghafla ambayo husababisha kupoteza Maisha.

“Mazoezi ni kitu kizuri ila kapimeni afya zenu kabla ya kuanza hii itawasaidia katika kuimarisha afya na kujiepusha na magonjwa ambayo yanaweza kuepukika,”amesema Prof Janabi.
 
 
Katika hatua nyingine,Hospitali ya Taifa ya Muhimbili iko mbioni kuanza kutoa huduma za upandikizaji mimba kwa mashine maalum (IVF - In vitro Fertilization).
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Mohamed Janabi alisema kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imekamilisha ununuzi wa mashine za kusaidia upandikizaji mimba zilizogharimu shilingi bilioni 1.

“Huduma za upandikizaji mimba zitaanza kutolewa hivi karibuni baada ya kamilisha usimikaji wa mitambo ya kutolea huduma hizo,”amesema Prof. Janabi.

Prof. Janabi ameeleza kuwa, tatizo la watu kutopata ujauzito ni kubwa na Watanzania wengi wamekuwa wakitoka nje ya nchi kupata huduma za kupandikizwa mimba kwa gharama kubwa, hivyo Serikali imesogeza huduma hizo karibu hivyo zitaanza kupatikana hapa hapa nchini.

“Jengo lilishakamilika na Muhimbili tulitenga chumba cha kutolea huduma hizo na kwa sasa tunasubiri usimikaji wa mitambo hiyo ikamilike ndiyo tuanze kutoa huduma hizo, na wananchi wanaohitaji huduma hizo hawatakwenda nje ya nchi kupata huduma hizo,”ameeleza Prof. Janabi.

Prof. Janabi amesema kuwa, hospitali tayari ina wataalamu waliowezeshwa na mafunzo ya utoaji wa huduma hiyo na wamesharejea kutoka masomoni, hivyo kusubiri kuanza kwa kutolewa kwa huduma hizo.

Aidha, amesema kuwa wataanza na kliniki za kawaida kisha hatua za upandikizaji zitafutwa kwa kushirikiana na wataalamu elekezi kutoka nje ya nchi ili kufanikisha huduma za upandikizaji mimba ambao wataelendelea kuwajengea uwezo wataalam wa hospitali hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news