Rais Dkt.Samia aendelea kurejesha tabasamu kwa wazee na yatima

ZANZIBAR-Mkuu wa Wilaya ya Kusini, Rajab Yussuf Mkasaba kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan ameendelea kutoa vyakula na mahitaji mengine kwa wazee na yatima kwa Shehia za Muyuni A,B,C.
Misaada hiyo imetolewa na Mheshimiwa Rais Dkt.Samia kwa Shehia zote 21 za Wilaya ya Kusini Unguja.
Kwa nyakati tofauti, wananchi waliofikiwa na misaada hiyo ya Mheshimiwa Rais licha ya kumpongeza kwa moyo wake wa upendo kwa makundi mbalimbali nchini, pia wamesema wataendelea kumuombea afya njema, hekima na maarifa ili azidi kuiongoza Tanzania kwa mafanikio zaidi.
Mheshimiwa Rais amefanya hivyo, ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za Wiki ya Tamasha la Kizimkazi ambalo ndiye mwasisi wake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news