Rais Dkt.Samia ashiriki Maadhimisho ya Miaka 60 ya KKKT

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) akipata maelezo kuhusu Maabara za Sayansi za Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira Mkoani Arusha mara baada ya kuzifungua rasmi kwenye Maadhimisho ya miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) yaliyofanyika katika Viwanja vya Mfuko wa Wastaafu Mkoani Arusha tarehe 21 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia kazi mbalimbali za Kanisa alipotembelea Maonesho Maalum kwenye Maadhimisho ya miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) yaliyofanyika katika Viwanja vya Mfuko wa Wastaafu Mkoani Arusha tarehe 21 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Fredrick Shoo alipowasili katika Viwanja vya Mfuko wa Wastaafu kwa ajili ya kushiriki Maadhimisho ya miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Mkoani Arusha tarehe 21 Agosti, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) pamoja na Waumini wa Kanisa hilo, kwenye Maadhimisho ya miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) yaliyofanyika katika Ukumbi wa Viwanja vya Mfuko wa Wastaafu Mkoani Arusha tarehe 21 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe pamoja na Maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kuashiria ufunguzi rasmi wa Maabara za Sayansi za Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira kwenye Maadhimisho ya miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) yaliyofanyika katika Viwanja vya Mfuko wa Wastaafu Mkoani Arusha tarehe 21 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungua kitambaa pamoja na Maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kuashiria ufunguzi rasmi wa Maabara za Sayansi za Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira kwenye Maadhimisho ya miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) yaliyofanyika katika Viwanja vya Mfuko wa Wastaafu Mkoani Arusha tarehe 21 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Maaskofu na Viongozi mbalimbali wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) wakati alipowasili katika Viwanja vya Mfuko wa Wastaafu Mkoani Arusha kwa ajili ya kufungua Maabara za Sayansi za Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira kwenye Maadhimisho ya miaka 60 ya Kanisa hilo tarehe 21 Agosti, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Shada la maua kutoka kwa mtoto Evynne Anicet Maganya (9) Mkazi wa Arusha, wakati alipowasili katika Viwanja vya Mfuko wa Wastaafu Mkoani Arusha kwa ajili ya kufungua Maabara za Sayansi za Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira kwenye Maadhimisho ya miaka 60 ya Kanisa hilo tarehe 21 Agosti, 2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news