Sekretarieti ya TNCM yakutana na Katibu Mkuu Dkt.Yonazi

DAR ES SALAAM-Mwenyekiti wa Kamati ya Uratibu wa Fedha za Mfuko wa Dunia kwa ajili ya Kudhibiti UKIMWI, Malaria na Kifua Kikuu (TNCM) ambaye pia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonazi amekutana na sekretarieti ya kamati hiyo leo Agosti 23,2023 katika kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Kikao hicho kimejikita katika kujengeana uelewa wa pamoja kuhusu uratibu wa programu za Malaria, Kifua Kikuu, UKIMWI pamoja Uimarishaji wa Mifumo ya kutolea Huduma za Afya nchini kupitia ufadhili wa Mfuko wa Dunia (Global Fund).
Wengine walioshiriki katika kikao hicho ni Katibu Mtendaji wa TNCM, Dkt.Rachel Makunde, Bw.Paul Sangawe ambaye ni Mkurugenzi wa Sera na Uratibu wa Shughuli za Serikali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Pamoja na Maafisa kutoka OWM na Sekretarieti ya TNCM.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news