Serikali kuanza kutumia Mfumo mpya wa Usimamizi wa Madeni

NA FARIDA RAMADHANI-WF

SERIKALI imeungana na nchi nyingine za Jumuiya ya Madola kwa kuanza kutumia Mfumo mpya wa Usimamizi wa Madeni (CS-Meridian) ambao utaboresha upatikanaji wa taarifa za madeni.   
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Omolo (katikati), Meneja MradiTaasisi ya Usimamizi wa Uchumi Mpana na Sekta ya Fedha Mashariki na Kusini mwa Afrika (MEFMI), Bi. Josephine Tito (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Madeni, Uchumi, Vijana na Maendeleona Mshauri wa Jumuiya ya Madola, Bw. Mac Banda, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Wizara hiyo, wajumbe kutoka Sekretariet ya Jumuiya ya Madola, Serikali ya Zanzibar pamoja na Benki Kuu ya Tanzania baada ya uzinduzi wa Mfumo mpya wa Usimamizi wa Madeni (CS-Meridian), jijini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Fedha na Mipango wakifuatilia mawasilisho mbalimbali kabla ya kuzinduliwa kwa Mfumo mpya wa Usimamizi wa Madeni (CS-Meridian), jijini Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dodoma).

Akizungumza jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa mfumo huo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Omolo amesema mfumo huo utaleta tija katika kuhifadhi taarifa za madeni pamoja na kuongeza uwazi wa takwimu za madeni hayo. 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Omolo, akizungumza kabla ya kuzindua rasmi Mfumo mpya wa Usimamizi wa Madeni (CS-Meridian) ambao Tanzania imejiunga rasmi ili kuboresha usimamizi wa taarifa za madeni, jijini Dodoma. 

“Wizara ya Fedha imeona ni muhimu kuingia kwenye mfumo mpya wa Kimataifa ambao unatumiwa na wenzetu katika Jumuiya ya Madola,"alibainisha Bi. Omolo. 

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mwandamizi wa Kurugenzi ya Uchumi, Vijana na Maendeleo Endelevu katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola, Dkt. Ruth Kattamuri, ambaye alishiriki uzinduzi huo kwa njia ya mtandao, aliipongeza Serikali ya Tanzania kuingia katika mfumo huo na kuahidi kuwa jumuiya hiyo itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuhakikisha mfumo huo unafanya kazi kwa ufanisi na kuleta maendeleo. 
Kamishna Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Madeni Wizara ya Fedha, Bw. Omary Khama, akizungumza kuhusu Mfumo mpya wa Usimamizi wa Madeni (CS-Meridian), katika uzinduzi uliofanyika katika ukumbi wa Treasury Sruare, jijini Dodoma.
Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Madeni, Uchumi, Vijana na Maendeleo na Mshauri katika Jumuiya ya Madola, Bw. Mac Banda, akizungumza kuhusu Mfumo mpya wa Usimamizi wa Madeni (CS-Meridian), kabla ya kuzinduliwa rasmi, jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Jenifa Omolo, akizungumza jambo na Kamishna Msaidizi Idara ya Usimamizi wa Madeni Wizara ya Fedha, Bw. Omary Kama (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Madeni, Uchumi, Vijana na Maendeleo na Mshauri katika Jumuiya ya Madola, Bw. Mac Banda (kushoto), baada ya kuzinduliwa kwa Mfumo mpya wa Usimamizi wa Madeni (CS-Meridian), jijini Dodoma.

Awali akiulelezea mfumo huo, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Usimamizi wa Madeni kutoka Wizara ya Fedha, Bw. Omary Khama, alisema mfumo huo ulitengenezwa na Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola mwanzoni mwa mwaka 2019. 

Alisema, Tanzania ilianza taratibu za kuhamia katika mfumo huo kuanzia mwezi June 2022 kwa kutumia wataalam wa ndani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news