Songwe wapewa huduma ya macho bila malipo

SONGWE-Serikali kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa Hellen Keller wamejipanga kuendelea kuboresha huduma za afya ya macho kwa kusogeza karibu huduma za mkoba za upasuaji wa mtoto wa jicho kwa wananchi wilayani Songwe bila malipo.

Hayo yamebainishwa na Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe, Dkt.Calvin Mwashi katika kambi ya uboreshaji wa huduma ya afya ya macho kwa kufanya upasuaji wa mtoto wa jicho ambao imeanza Agosti 4, 2023 mpaka Agosti 7, 2023 katika Hospitali ya Wilaya ya Songwe mkoani Songwe.

Dkt.Mwashi amesema, huduma hiyo ambayo inalenga kuwaisaidia wananchi wote wenye uhitaji na walioshindwa kumudu gharama ya huduma kwa kutibiwa bila malipo kupitia mradi huo wa huduma ya upasuaji wa mtoto wa jicho.

Hata hivyo, Dkt.Mwashi ameelezea umuhimu wa mradi huo ni pamoja na kuwajengea ujuzi wauguzi na wataalamu wa Hospitali hiyo ya wilaya ambao wameshiriki katika kuwahudumia wananchi wa wilaya hiyo.

Ametoa wito kwa wananchi wote wenye tatizo la mtoto wa jicho au wenye viashiria vya tatizo hilo kujitokeza ili kupata huduma hiyo ya upasuaji wa mtoto wa jicho ambayo haina malipo ili kuwanusuru na upofu.

Dkt.Mwashi amewashukuru wadau wa sekta ya afya kwa namna wanavyojitoa katika kuwaisaidia wananchi katika sekta ya afya ili kutoa huduma bora ya Afya kwa wananchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Helen Keller, Dkt.Deogratius Ngoma amewataka wadau wa sekta ya afya kuungana kwa pamoja na kushirikiana na serikali ili kusaidia kuboresha huduma bora za Afya kwa wananchi ambao wameshindwa kumudu gharama za huduma hizo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news