Serikali yatoa maagizo kwa Menejimenti ya Hifadhi ya Taifa Katavi

KATAVI-Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja ameitaka Menejimenti ya Hifadhi ya Taifa Katavi kuainisha maeneo ya uwekezaji huku akisisitiza utangazaji wa kimkakati katika maeneo hayo ufanyike ili kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje nchi kuwekeza katika hifadhi hiyo.
Ametoa kauli hiyo leo wakati alipofanya ziara ya kikazi katika Ofisi za Makao Makuu ya Hifadhi hiyo, ambapo amesema utangazaji wa maeneo hayo utawavutia Wawekezaji kuwekeza katika ujenzi wa huduma za malazi ya watalii.

"Ainisheni maeneo hayo kwani Wawekezaji wengi wanataka kuwekeza katika hifadhi hii," Mhe. Masanja amesisitiza.
Akizungumzia faida ya kutangaza maeneo watakayoainisha, Mhe.Masanja amesema miundombinu itaboreka pamoja na mazingira yatawavutia watalii wengi kuja kutembelea na kulala hifadhini humo.

Katika hatua nyingine, Mhe.Masanja ameendelea kuwasisitiza Wananchi kuacha kuvamia maeneo ya Hifadhi huku akiwataka wahifadhi kuendelea kuelimisha wananchi juu ya umuhimu wa maeneo hayo kitaifa na kimataifa.
"Ili kuendelea kuwa na mahusiano mazuri na Wananchi wetu, Nawaomba nendeni mkatoe elimu kwa wananchi wasisogelee maeneo ya hifadhi na hapo walipo wasiendelee kuongeza maeneo," Mhe. Masanja amesema.

Hifadhi ya Taifa Katavi ni hifadhi ya tano kwa ukubwa kati ya hifadhi 21 nchini ikiwa na kilomita za mraba 4,471.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news