T-PESA itakuwa zaidi ya pesa

NA GODFREY NNKO

SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limesema kuwa, kwa sasa limejielekeza kupeleka huduma yake ya T-PESA kwenye maeneo ambayo hayana mvuto kibiashara nchini.

Dhamira ni kuhakikisha kuwa, Watanzania wote wanapata huduma bora na kwa wakati iwe mijini au vijijini kupitia shirika lao ambalo lipo mstari wa mbele kuboresha maisha yao kupitia huduma za mawasiliano.

Mkurugenzi wa T-PESA,Bi.Lulu Mkudde ameyaeleza hayo leo Agosti 24, 2023 jijini Dar es Salaam wakati wa kikao kazi na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari, kinachoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina ambapo leo ilikuwa ni zamu ya TTCL kuelezea walipotoka, walipo na wanapokwenda.

"Pia T-PESA imejielekeza kupeleka huduma kwenye maeneo ambayo hayana mvuto kibiashara, katika hayo maeneo pia T-PESA inaingia kwenye mfumo wa malipo."

Pia,Mkurugenzi huyo amefafanua kuwa,shirika hilo kupitia huduma ya T-PESA limedhamiria kuendeleza mageuzi makubwa ya teknolojia ya kidigitali ili kumuwezesha kila mwananchi aweze kupata huduma za kifedha nchini.

"Kama mtoa huduma wa kidigitali ili kuchangia kuendeleza ukuaji wa uchumi kupitia fedha za simu kwa kurahisisha malipo hayo kwa njia ya mtandao kama vile kufanikisha malipo ya kaya zisizo na uwezo TASAF na malipo ya wakulima.

"Lakini pia kusaidia mpango wa maendeleo katika sekta ya fedha Tanzania katika hatua ambayo TTCL imechukua kuhakikisha T-PESA inapiga hatua ni kuangalia bidhaa ambazo inakuja nazo.

"Na moja ni kama mlivyoona mteja wetu anaweza kufungua T- PESA bila kuwa hata na simu-card kama ambavyo tumezoea mteja akiwa na simu janja anaweza aka-download app ya T-PESA na moja kwa moja akafungua akaunti yake.

"Huduma hii ni huduma unique na inamwezesha mtu kufungua akaunti hiyo popote alipo. Lakini pia kutoa huduma ya M-Card,"amefafanua Mkurugenzi wa T-PESA,Bi.Lulu Mkudde.

Amesema, huduma hiyo kwa sasa amesema, inatumika katika Stendi ya Magufuli. "Na, wale mashabiki wa mpira mpaka sasa tangu kuanzishwa huduma hii 2020 tuna wateja zaidi ya milioni 2.9 ambao wanatumia huduma hizi za M- Card, hii inaonesha ufanisi wa mfumo huu na jinsi unavyokua kwa kasi."

"Na matarajio yetu ni kuendelea kukuza huduma zetu, tulileta suluhisho upatikanaji wa vocha za TTCL, kipindi cha nyuma zilikuwa na changamoto watu walikuwa wakilalamika kwa nini hatuleti vocha T-PESA ikaja na mkakati wa kuhakikisha inakuja na upatikanaji wa vocha kupitia T-PESA,"amefafanua.

Mkurugenzi wa T-PESA,Bi.Lulu Mkudde ameendelea kufafanua kuwa,pia katika miaka minne ijayo wamejikita zaidi katika kuhakikisha kwamba T- PESA inakuwa nguzo ya miamala ya kifedha.

"Ni kwa njia ya kielektroniki katika kuhakikisha inafanya utekelezaji wa kubuni na kuanzisha miradi mbalimbali nchini.

"Itaongeza juhudi za Serikali kwa kukuza uchumi wa kidigitali katika masuala ya afya, kifedha, elimu na taarifa za masoko ambayo ipo katika mpango mkakati wa miaka mitano.

"Kampuni imepanga kusajili wateja ambao imeshakubaliana nao, kuongeza idadi ya matumizi ya intaneti kufikia asilimia 20 ya malengo yake ambayo imejiwekea, kuongeza watoa huduma wa lipa kwa T-PESA."

"Lakini pia tunataka kuongeza wigo wa platform ya T-PESA kuongeza vyanzo vya mapato zaidi,"amesisitiza Mkurugenzi wa T-PESA,Bi.Lulu Mkudde.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news