Mkombe Luxury Bus waanza safari kutoka Dar es Salaam hadi Afrika Kusini kwa nauli kidogo

JOHANNESBURG/DAR ES SALAAM-Habari njema na za kufurahisha kwa sasa watanzania wanaweza kusafiri kwa raha mustaree kwa usafiri wa basi kutoka Dar Es Salaam hadi Johannesburg,Afrika Kusini kwa kutumia mabasi mapya kabisa aina ya kampuni ya kizalendo ya Kitanzania Mkombe Luxury Bus ambayo ina makao yake Johannesburg nchini Afrika Kusini.
Kampuni hiyo ya kitanzania imekuja na suluhisho la kurahisisha Safari za kutoka hapa nchini hadi Afrika Kusini,kwa sasa wasafiri wa Tanzania na Afrika Kusini wanaweza kutumia usafiri huo wa Mkombe Luxury Bus ambao nauli yake ni Tsh 350,000 za kitanzania kwa safari moja na wanaweza kulipia nauli ya Tsh,700,000 (laki saba) kwenda na kurudi.
Kampuni hiyo imefungua ofisi zake Mtaa wa Shekilango jijini Dar es Salaam alaam ambapo tiketi zinapatikana, pia wanapatikana kwa WhatsApp +27604749717.

Wasafiri wa Tanzania na South Africa wanaweza kutumia usafiri kwa kupitia Zambia, maporomoko ya maji ya Victoria Falls, Zimbabwe hadi Johannesburg nchini Afrika Kusini na basi linachukua siku tatu hadi Afrika kusini.
Kampuni hiyo ya kizalendo Mkombe imekuja kurahisisha ufasari wa kwenda na kurudi hadi Afrika Kusini na pia wana magari magari ya kusafirisha mizigo.

Safiri kwa Raha na Mkombe Luxury Bus ambayo ndani kuna huduma ya Choo,TV na WiFi ya Internet safarini kote. Watanzania wanaposafiri na usafiri huu Luxury Mkombe Bus ni Utalii Tosha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news