Tanzania yafungua rasmi ubalozi jijini Algiers

ALGIERS-Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefanya ufunguzi rasmi wa Ubalozi wake Agosti 2,2023 jijini Algiers nchini Algeria.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akikata utepe kuashiria ufunguzi wa ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria tarehe 2 Agosti 2023 jijini Algiers. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Diaspora wa Algeria, Mhe. Ahmed Attaf na kulia ni Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Meja Jenerali (Mst) Jacob Kingu wakishuhudia ufunguzi huo.

Ufunguzi huo umefanywa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) na kuhudhuriwa na mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya Nje na Diaspora wa Algeria, Mhe. Ahmed Attaf, Balozi wa kwanza wa Algeria kuhudumu nchini Tanzania, Balozi Noureddine Djoudi na Jumuiya ya Wanadiplomasia nchini Algeria.

Viongozi wengine waliohudhuria ufunguzi huo ni Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. Seif Shekalaghe, Naibu Makatibu Wakuu kutoka Wizara za Elimu, Sayansi na Teknolojia, Nishati na Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Waziri wa Mambo ya Nje na Diaspora wa Algeria, Mhe. Ahmed Attaf wakiwa katika ufunguzi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria tarehe 2 Agosti 2023.

Akihutubia kwenye ufunguzi wa Ubalozi huo Waziri Tax ameeleza kuwa Tanzania na Algeria zimejidhatiti kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kwa lengo la kukuza ushirikiano wenye maslahi kupitia sekta za kipaumbele.

‘’Ni imani yangu kuwa Ubalozi huu utaendelea kuwa kiunganishi kati ya serikali zetu kwa kutoa huduma za kidiplomasia, kuhudumia Watanzania,”alisema Dkt.Tax.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akipongezwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Diaspora wa Algeria, Mhe. Ahmed Attaf baada ya kukamilisha taratibu za ufunguzi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria tarehe 2 Agosti 2023.

Naye Mhe. Attaf ameeleza kuwa ziara ya Waziri Tax imekuwa na mafanikio makubwa kwa kuwa wamepata fursa ya kuzungumza masuala ya ushirikiano katika sekta za biashara, uwekezaji na sekta nyingine muhimu kwa maendeleo ya mataifa hayo mawili.

‘’Balozi zetu zitaendelea kutekeleza majukumu yake ya msingi ili nia ya dhati ya kuimarisha na kukuza uhusiano iweze kuleta tija zaidi na kuziwezesha nchi zetu kunufaika kiuchumi,’’ alisema Mhe. Attaf.

Ufunguzi wa Ubalozi umefanyika pembezoni mwa Mkutano wa Tano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Algeria ambao umemalizika kwa mafanikio na kuwezesha kusainiwa kwa Hati 8 za Makubaliano ya Ushirikiano katika sekta za nishati, mafuta na gesi, elimu na teknolojia, mafunzo ya diplomasia, kumbukumbu na nyaraka, ulinzi na usalama, ushirikiano wa kidiplomasia, kilimo na afya. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Diaspora wa Algeria, Mhe. Ahmed Attaf akihutubia wakati wa hafla ya ufunguzi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria tarehe 2 Agosti 2023.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo (mwenye tai ya bluu) akifatilia hotuba zilizowasilishwa na Mawaziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Dkt. Tax na na Mhe. Attaf.
Kutoka Kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Naimi Aziz, Mkurugenzi Mkuu Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Diaspora ya Algeria, Balozi Selma Malika na Balozi Djoudi wakifuatilia hafla ya ufunguzi huo.
Picha ya pamoja, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Waziri wa Mambo ya Nje na Diaspora wa Algeria, Mhe. Ahmed Attaf.
Picha ya Pamoja, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax, Waziri wa Mambo ya Nje na Diaspora wa Algeria, Mhe. Ahmed Attaf na Watumishi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria na ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa Tano wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPC) kati ya Tanzania na Algeria.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akimkabidhi zawadi Balozi wa kwanza wa Algeria kuhudumu nchini Tanzania, Balozi Noureddine Djoudi wakati wa hafla ya ufunguzi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Stergomena Tax akihutubia wakati wa hafla ya ufunguzi wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria tarehe 2 Agosti 2023.

Uhusiano kati ya Algeria na Tanzania uliasisiwa mwaka 1963 mara baada ya uhuru wa Tanganyika. Tangu wakati huo nchi hizi zimeendelea kushirikiana katika maeneo mbalimbali kwa maslahi ya pande zote. 

Vilevile katika kuimarisha ushirikiano huo Tanzania imefanya ufunguzi wa Ubalozi wake nchini Algeria ambao ulianza kutekeleza majukumu yake tangu mwaka 2017.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news