Waziri Prof.Mbarawa asisitiza jambo Kigoma

KIGOMA-Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amezungumzia umuhimu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kujenga mizani katika barabara kuu zinazoingia na kutoka mjini Kigoma.
Amesema kasi ya ujenzi wa barabara za kisasa mkoani Kigoma ni vema ikaendana na ujenzi wa mizani za kudhibiti uzito ili kuzilinda barabara hizo.

"TANROADS hongereni kwa kusimamia kwa karibu miradi ya ujenzi wa barabara inayoendelea katika mkoa huu, ni muhimu sasa muanze kujenga mizani ili kukamilika kwa barabara hizi kuendane na kuzilinda dhidi ya magari yanayozidisha uzito," amesema Prof. Mbarawa.

Barabara kuu za Nyakanazi-Kigoma na Kigoma-Tabora ziko kwenye hatua muhimu za kukamilika kwa kiwango cha lami na hivyo kuvutia biashara na kukua kwa huduma za uchukuzi hivyo uwepo wa mizani za kisasa utasaidia kuzilinda barabara hizo ili zidumu kwa muda mrefu.

Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa amekagua ujenzi wa barabara ya Nduta Junction-Kibondo Mjini hadi Kibondo Junction yenye urefu wa KM 25 na Malagarasi-Ilunde KM 51.1 zinazojegwa na mkandarasi STECOL Cooperation Limited na kumtaka mkandarasi huyo kuongeza idadi ya vifaa na wataalam ili kasi ya ujenzi wa barabara hizo uendane na mahitaji ya Serikali ya kuufungua mkoa wa Kigoma kwa lami mapema iwezekanavyo mwakani.

"Hakikisheni mnaongeza kasi katika ujenzi huu Serikali haitasita kuwaondoa ikiwa mtashindwa kukamilisha kazi kwa wakati,,"amesisitiza Prof. Mbarawa.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Dinah Mathamani amesema, wilaya itaendelea kutoa ushirikiano kwa mkandarasi kadri anavyohitaji ili kukamilisha ujenzi huo.

Prof.Makame Mbarawa alikuwa katika ziara ya siku tatu kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi ya miundombinu ya barabara na bandari.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news