USAID yaahidi ushirikiano zaidi nchini

DODOMA-Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la Misaada la Marekani (USAID), Craig Hart ameahidi kuendeleza ushirikiano uliopo kati ya shirika hilo na Tanzania kuhakikisha ustawi wa watoto unaimarishwa.
Craig ameyasema hayo alipokutana na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt.Dorothy Gwajima jijini Dodoma Agosti 21, 2023 kwa lengo la kujitambulisha na kuanza majukumu yake nchini baada ya aliyekuwepo Cate Somvogsiri kumaliza muda wake.

Craig amesema suala la malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto linahitaji ushirikiano wa wadau wote hivyo kuahidi kuwaunganisha wadau kufanya kazi kwa pamoja.
Kwa upande wake Waziri Dkt. Gwajima amemueleza Mkurugenzi huyo kwamba katika kuhakikisha huduma bora za Ustawi hasa kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu, Wizara inashirikiana na USAID tangu mwaka 2013 kupitia miradi mbalimbali.
Ameongeza kuwa, bado kuna changamoto kadhaa zinazohitaji ushirikiano ili kuzitatua baadhi zikiwa ni migogoro ya familia, uhaba wa Maafisa Ustawi wa Jamii na upungufu wa vitendea kazi kwa Maafisa hao.
"Juhudi za pamoja zilizofanywa katika uimarishaji wa mfumo na utoaji wa huduma kwa watoto walio katika mazingira hatarishi zimefanya kuongeza ubora unaozingatia matokeo na mabadiliko katika maisha ya walengwa na kuleta matumaini na ustawi kwenye jamii,"amesema Dkt. Gwajima.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news