Vikao vya kamati za Bunge kuanza Dodoma

DODOMA-Vikao vya kawaida vya Kamati za Kudumu za Bunge vitaanza kufanyika Jumatatu tarehe 14 hadi 25 Agosti, 2023 jijini Dodoma kwa ajili ya maandalizi ya Mkutano wa Kumi na Mbili wa Bunge utakaonza tarehe 29 Agosti, 2023.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Agosti 6,2023 na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa,Ofisi ya Bunge jijini Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kamati tano zitatangulia kuanza vikao, ambapo nne kati ya hizo zitaanza vikao tarehe 07 Agosti, 2023, na Kamati moja (Bajeti) itaanza tarehe 10 Agosti, 2023.

Shughuli za Kamati katika kipindi hicho zitakuwa ni: -

i) Uchambuzi wa Miswada miwili (2) ya Sheria utakaofanywa na Kamati mbili: Kamati ya Utawala, Katiba na Sheria na Kamati ya Bajeti;

ii) Uchambuzi wa Sheria Ndogo zilizowasilishwa wakati wa Mkutano wa Kumi na Moja wa Bunge;

iii) Uchambuzi wa Taarifa za Hesabu zilizokaguliwa na CAG kwa Mwaka wa Fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2022;
 
iv) Uchambuzi wa Taarifa za Uwekezaji wa Mitaji ya Umma kwa lengo la kuliwezesha Bunge kufuatilia ufanisi na tija kwa Mitaji ya Serikali kwenye mashirika mbalimbali na taasisi; na

v) Uchambuzi wa Taarifa za Utendaji za Wizara kwa lengo la kuliwezesha Bunge kutekeleza jukumu la kuisimamia na kuishauri Serikali. Ratiba ya shughuli za Kamati pia inapatikana katika Tovuti ya Bunge ambayo ni www.parliament.go.tz

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news