Wamshirikisha Mbunge Prof.Muhongo hitaji lao

NA FRESHA KINASA

WANANCHI wa Masinono katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma mkoani Mara wameiomba Serikali isaidie kutatua changamoto ya mawasiliano waliyonayo kwa kuweka minara ya simu kusudi wawe na uhakika wa huduma hiyo muhimu.

Hayo wamemweleza Mbunge wa jimbo hilo, Prof.Sospeter Muhongo katika mkutano alioufanya na wananchi hao. Ambapo pamoja na mambo mengine wamepongeza maendeleo yanayofanywa na Mbunge wao chini ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Baadhi yao wamesema kuwa, kuna baadhi ya laini hazishiki na hivyo mawasiliano kutokuwa thabati hivyo utatuzi wa jambo hilo utakuwa na faraja kwao.

"Tutashukuru sana Mheshimiwa Mbunge wetu akisaidia kuimarisha mawasilino, kwani baadhi ya laini hazishiki.

"Mbunge wetu amekuwa akifanya makubwa ambayo wana Musoma Vijijini tunayaheshimu na kuyathamini wakati wote yameleta mabadiliko jimboni mwetu. Na hili pia tunaamini analiweza,"amesema mmoja wa wananchi wa Masinono.

Naye Fabian Maira amesema kwamba, mawsiliano ni nyenzo muhimu ya maendeleo, hivyo ufumbuzi wa jambo hilo litakuwa na tija kwa wananchi wa Masinono ambao ni wakulima na wafugaji.

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo akizungumzia jambo hilo amesema, tayari ameshawasilisha ombi maalumu la kuweka minara katika maeneo yenye changamoto ya upatikanaji wa mitandao.

"Minara ya simu wametupatia michache, nimeomba angalau waweke mnara mpya kwenye kijiji cha pembezoni, sasa yale mawimbi kama vijiji vya pembezoni vikizunguka itakuwa vizuri sana kwa hiyo nayo inakuja,"amesema Prof. Muhongo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news