Huduma bora za afya ni malengo ya Serikali-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema, malengo ya Serikali katika sekta ya afya ni kuhakikisha wananchi wa Zanzibar wanapata huduma bora za afya.

Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo Agosti 14,2023 wakati akifungua Kituo cha afya Bumbwini Makoba, Wilaya ya Kaskazini B Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi alieleza katika hatua za awali zinazofanywa na Serikali katika sekta ya afya ni kuhakikisha wananchi wa Zanzibar wanapata huduma bora kufikia malengo ya kuimarisha miundombinu kwa kujenga hospitali za wilaya kila wilaya.

Sambamba na hospitali za mkoa kila mkoa na Hospitali ya Binguni itakayokuwa kubwa zaidi na kutoa huduma za uchunguzi Zanzibar.

Wakati huo huo,Serikali imeamua kushirikiana na sekta binafsi zitoe huduma katika hospitali za serikali zinazohusisha uchunguzi wa maradhi mbalimbali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news