Ajali yaua mashabiki wa Namungo FC

LINDI-Mashabiki wanne wa Namungo FC kutoka mkoani Lindi inadaiwa wamefariki dunia kutokana na ajali waliopata wakiwa njiani kwenda kuishabikia timu hiyo.

Uongozi wa Namungo FC ya Ruangwa mkoani Lindi umeeleza kuwa, gari la mashabiki wake lililokuwa linatoka Lindi kwenda Dar es Salaam kuishangilia timu hiyo katika mchezo dhidi ya Yanga SC limepata ajali na mashabiki hao kufariki na 16 kujeruhiwa.

Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa, mashabiki hao waliokuwa wanatoka Lindi ili kuwahi mchezo huo leo Septemba 20,2023 saa 1:00 usiku katika uwanja wa Azam Complex uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa mashabiki hao wamepata ajali katika eneo la Miteja karibu na Somanga.“Kwa sasa majeruhi wamepelekwa katika Kituo cha Afya Tingi Wilaya ya Kilwa Mkoa wa Lindi, Namungo FC inatoa pole kwa wafiwa na tunawaombea majeruhi wapone haraka,”imefafanua sehemu ya taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news