Ajali yaua, yajeruhi sita

MOROGORO-Mtu mmoja amefariki dunia na wengine sita wamejeruhiwa katika ajali ya gari iliyohusisha magari mawili moja likiwa lori la mizigo na basi la abiria aina ya Tata.
Akizungumzia tukio hilo Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro, Emmanuel Ochieng amesema, chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa gari la mizigo (Lori) kwa kutozingatia alama na michoro ya usalama wa barabarani iliyokuwepo katika eneo hilo.

Amefafanua, lori lilikuwa likitokea uelekeo wa Msamvu na kuelekea uelekeo wa Iringa na basi la abiria lililokuwa likitokea Ifakara likielekea katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Msamvu Morogoro na kwamba ajali hiyo imetokea barabara kuu ya Morogoro-Iringa Manispaa ya Morogoro.

Pia Kamanda Ochieng amesema, anayesadikiwa kupoteza maisha katika ajali hiyo ni dereva wa lori na mwili wake umehifadhiwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro na wengine sita ambao ni majeruhi walikuwa kwenye basi la abiria na hadi sasa wanaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news