DC Makilagi aridhishwa na utekelezaji Mradi wa maji Butimba, wafikia asilimia 96

MWANZA-Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe. Amina Makilagi amesema utekelezaji wa ujenzi wa mradi wa maji Butimba unakwenda vizuri na kasi inaridhisha.
Amesema hayo leo Septemba 12,2023 katika ziara yake na Kamati ya Usalama Wilaya Nyamagana kwenye mradi wa Maji Butimba akiwa ameambatana na Menejimenti ya MWAUWASA ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, ndugu Neli Msuya.

Ziara hiyo imelenga kujionea maendeleo ya mradi kuelekea siku ya majaribio ya awali ya mradi huo Septemba 15, 2023.

"Niwapongeze MWAUWASA kwa kazi nzuri na kasi hii ya utekelezaji mnayoendelea nayo, niipongeze pia timu iliyoundwa na Mhe. Jumaa Aweso, Waziri wa Maji kwa ushirikiano huu mnaoutoa kwa MWAUWASA, tuna imani tutapata matokeo chanya," amesema Mhe. Makilagi.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) Ndg. Neli Msuya amesema utekelezaji wa mradi sasa umefikia asilimia 96 na kuongeza kuwa majaribio ya mradi yatakayoanza tarehe 15 Mwezi Septemba ni hatua ya awali kuelekea katika hatua ya ukamilishwaji.

"Tunakwenda kwa awamu, majaribio haya yatatupa matokeo chanya katika upatikanaji wa huduma ya Maji kwa awamu. Wananchi wataanza kuona mabadiliko kadri siku zinavyokwenda,"amesema Neli.

Mradi wa Maji Butimba unatekelezwa kwa gharama ya Tsh. Bilioni 69 na utazalisha kiasi cha lita milioni 48 kwa siku na utahudumia zaidi ya wakazi 450,000.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news