Ligi Kuu ya NBC kila mmoja anataka ushindi

KAGERA/KIGOMA-Kagera Sugar FC imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.

Ni mtanange uliopigwa Septemba 17, 2023 katika Dimba la Kaitaba ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.

Disan Galiwango dakika ya 90 ndiye aliyewapa raha Kagera Sugar ikiwa ni ushindi wa kwanza kwao baada ya kufungwa mechi mbili za awali.

Awali Mashujaa FC waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara ambao ulipigwa Lake Tanganyika mkoani Kigoma.

Omary Kindamba dakika ya 18 na Adam Adam dakika ya 80 ndiyo waliowawezesha wenyeji hao wa Kigoma ambao walipanda daraja msimu huu kupata matokeo mazuri.

Aidha, Mashujaa FC wanafikisha alama saba katika mchezo wa tatu na kupanda kileleni mwa Ligi Kuu wakizizidi alama moja moja kwa Simba SC, Yanga SC na Azam FC.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news