Ligi ya NBC Championship yapamba moto

ARUSHA-Timu za TMA ya Arusha, Ken Gold ya Mbeya na Copco FC ya Mwanza zimefanikiwa kushinda michezo yao kwenye Ligi ya NBC Championship kwa mara ya kwanza msimu huu.

TMA ilicheza mapema saa 8:00 mchana kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha na kushinda 1-0 dhidi ya Biashara ya Mara.

Ushindi huo umeifanya TMA kufikisha alama nne na kukaa nafasi ya nne ikiwa haijafungwa mchezo wowote mpaka sasa huku ikiwa mojawapo ya timu tatu zilizopanda daraja kutoka First League.

Ken Gold imeifunga Green Warriors ya Dar kwa bao 1-0 kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya na kufikisha alama nne zinazowaweka nafasi ya tatu huku wakiwa hawajapoteza mchezo mpaka mzunguko wa pili.

Kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Copco imepata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Cosmopolitan ya Dar I’m na kusogea mpaka nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi ya NBC Championship.

Cosmopolitan imeshindwa kupata alama yoyote mpaka mzunguko wa pili ikipoteza michezo yote miwili na kuruhusu jumla ya mabao saba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news