Mwalimu mbaroni kwa kuwaingiza watoto watano vidole sehemu za siri

NJOMBE-Mwanaume aliyejulikana kwa jina la Ngoitanile (60) ambaye ni mwalimu wa Shule ya Msingi Mwembetogwa iliyopo Mtila katika Kata ya Matola ndani ya Njombe Mji amekamatwa na polisi kwa tuhuma za ukatili.

Mwalimu huyo anatuhumiwa kuwaingiza vidole sehemu za siri watoto watano wanaosoma darasa la kwanza na la tatu na kuharibu usichana wao.

Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi mkoa wa Njombe ambaye pia ni Kaimu Kamanda Butusyo Mwambelo amethibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa mara baada ya kupata taarifa za uficho na kwenda kumkamata mwalimu huyo.

"Bahati nzuri tulikuwa na majina ya wale watoto ambao wako watano, wawili ni darasa la kwanza na watatu ni wa darasa la tatu.

"Kwa hiyo tukafanya utaratibu wa kuwapeleka hospitali na dakatari akatoa taarifa kwamba hao watoto inaonekana sehemu zao za siri wameingiliwa na kitu butu hawana bikira,"amesema Kamanda Mwambelo.

Amesema, mara baada ya taarifa hizo walilazimika kuwahoji watoto hao juu ya vitendo walivyofanyiwa ambapo waliweka wazi kuwa wamekuwa wakiingizwa vidole sehemu za siri na mwalimu huyo wakiwa darasani huku wakati mwingine akiwaita ofisini.

"Kibaya zaidi walipoulizwa wanafunzi wengine nao walikiri kweli kwamba huyu babu anafanya hicho kitendo mbele ya wanafunzi na lile darasa kuna watoto wa kiume na watoto wa kike.

"Kwa hiyo huyu mwalimu yupo hapa kituo cha polisi, lakini ushirikiano kwa walimu tumekosa wamesema hizo taarifa hawana ila watoto ndio wamesema,"ameongeza Kamanda huyo.

Aidha,Kamanda Butusio ametoa wito kwa wanannchi wa Mkoa wa Njombe kuacha kuficha taarifa za matukio kama hayo na kutoa ushirikiano kwa polisi.

Pia amebainisha kuwa, kwa sasa upelelezi unaendelea dhidi ya mtuhumiwa na hakuna dhamana itakayotolewa kwake kwa sasa mpaka mahakamani lakini sio kwa Jeshi la Polisi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

2 Comments

  1. Naomba serikali ituambie ni wapi ambapo ni sehemu salama kwa watoto wetu kupata elimu🤔🤔🤔❔

    ReplyDelete
  2. Alikuwa anatafuta nn huko alichokiifadhi. Daah walezi wetu tunawakabidhi kwa Mola

    ReplyDelete
Previous Post Next Post

International news