Mwanahabari Mathias Canal achangia milioni 4/- Shule ya Msingi Kiomboi Bomani

SINGIDA-Mwandishi wa habari,Mathias Canal amechangia madawati 30 yenye thamani ya shilingi milioni 2.1 na vitakasa mikono 20 vyenye thamani ya shilingi milioni 1.4.
Ametoa mchango huo Septemba 29, 2023 wakati akizungumza kwenye mahafali ya 60 ya Shule ya Msingi Kiomboi Bomani iliyopo katika Kata ya Kiomboi ndani Wilaya ya Iramba mkoani Singida.
Pamoja na mambo mengine pia Mathias amechangia kwa kutoa motisha ya shilingi 500,000 kwa ajili ya walimu katika shule hiyo kutokana na kazi nzuri wanayoifanya ya kuwafundisha wananfunzi shuleni hapo.
Kadhalika amesema kuwa, atawasomesha watoto wote watakaomaliza darasa la saba na kupata ufaulu wa alama ‘’A’’ kwa kila somo kuanzia wale waliohitimu mwaka huu 2023 katika shule hiyo.
Katika hatua nyingine amewapongeza wazazi na walezi wa wanafunzi shuleni hapo kwa kukubali kuchangia kwa hiari baadhi ya mahitaji ya wanafunzi ikiwemo chakula kwa ajili ya wanafunzi ambao wapo katika madarasa ya mitihani.
Ameongeza kuwa, wanafunzi hao bado hawajamaliza elimu ya darasa la saba mpaka pale watakapopata matokeo ya mitihani waliyoifanya, hivyo wazazi na walenzi wanapaswa kuendelea kuimarisha ulinzi na mwenendo bora wa malezi kwa watoto hao.
Wakati huo huo,Mathias Canal ameipongeza Serikali kwa kutoa shilingi milioni 40 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa pamoja na ofisi ya walimu.
Katika mahafali hayo, Mathias Canal aliambatana na Diwani wa Kata ya Kiomboi, Mhe. Omary Omary, na Mkurugenzi wa DM PLANET,David Mtengile ambaye amechangia 100,000 kwa ajili ya motisha kwa walimu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news