Naibu Waziri Byabato ateta na Waziri Smith jijini Havana

HAVANA-Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato (Mb.) amekutana na kuzungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Jamaica Mhe. Kamina John Smith pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kundi la G77+ China unaofanyika jijini Havana nchini Cuba.
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato (Mb.) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Jamaika Mhe. Kamina John Smith walipokuta pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kundi la G77+ China unaofanyika jijini Havana nchini Cuba tarehe 16 Septemba 2023.

Katika mazungumzo yao viongozi hao wameelezea kuridhishwa kwao na hali ya uhusiano wa kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na Jamaika na kuahidi kuendelea kushirikiana zaidi ili kuimarisha uhusiano huo.

Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Byabato amemuelezea Mhe. Smith kuwa Tanzania inaridhishwa na uhusiano mzuri uliopo na kuongeza kuwa kuna haja ya kuhakikisha uhusiano huo wa kidplomasia unaimarishwa na kufikia hatua ya juu.
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato (Mb.) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Jamaika Mhe. Kamina John Smith walipokuta pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kundi la G77+ China unaofanyika jijini Havana nchini Cuba tarehe 16 Septemba 2023.

Amemuhakikishia utayari wa Serikali ya Tanzania kuanzisha Tume ya Kudumu ya Pamoja (JPC) na Jamaika katika maeneo yatakayozinufaisha pande zote mbili.

Pia amemuelezea nia ya Tanzania kupanua wigo wa maeneo ya ushirikiano na kuingiza sekta za uchumi wa buluu, biashara na uwekezaji.
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato (Mb.) katika picha na Waziri wa Mambo ya Nje na Biashara wa Jamaika Mhe. Kamina John Smith baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kundi la G77+ China unaofanyika jijini Havana nchini Cuba tarehe 16 Septemba 2023.

Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Smith alisema pamoja na uhusiano mzuri uliopo kati yake na Tanzania, Jamaika inaiomba Tanzania kuiunga mkono katika nafasi mbili inazogombea kimataifa katika Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Bahari (IMO) na Kamati ya Urithi wa Dunia iliyo chini ya UNESCO.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news