Rais Dkt.Mwinyi ahutubia G77+China, asisitiza teknolojia na ubunifu

HAVANA-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amehutubia Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kundi la G77+ China akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kundi la G77+ China akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan jijini havana Cuba tarehe 15 Septemba 2023.
Akihutubia katika Mkutano huo, Dkt. Mwinyi amesema sayansi, teknolojia na ubunifu ni nguzo muhimu kwa nchi zinazoendelea kujiletea maendeleo ya kiuchumi na kuongeza kuwa nchi hizo zinaweza kuendelea kiuchumi kupitia maendeleo katika sekta muhimu za kilimo, nishati, elimu, afya, madini, maendeleo ya muindombinu, maji na mazingira. 

Mhe. Rais Dkt. Mwinyi amekumbusha namna nchi zinazoendelea zilivyoathirika na janga la maradhi ya UVIKO-19, bidhaa kupanda bei, mizozo ya kisiasa na athari za mabadiliko ya tabia nchi na kuongeza kuwa baadhi ya changamoto zilisababisha kupanda kwa gharama za maisha na kudhoofisha jitahada za kujikwamua kiuchumi.
Washiriki wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kundi la G77+ China wakifuatilia mkutano huo jijini Havana Cuba tarehe 15 Septemba 2023.

Mhe. Dkt. Mwinyi alikumbushia namna nchi zilizoendelea zilivyobanwa na teknolojia ya kutengeneza chanjo na kunyimwa msaada wa kiteknolojia ili zitengeneze chanjo zao na kusababisha kampuni za kutengeneza dawa za mataifa tajiri kupata faida kubwa kwa kuziuzia nchi zinazoendelea chanjo ya UVIKO-19.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Cuba Miguel Díaz-Canel mara baada ya kuwasili katika Ukumbi wa Mkutano wa 'Palacio De Convenciones De La Habana' jijini Havana Cuba,tayari kwa Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa kundi la G77na China.

Mhe.Dkt. Mwinyi amezitanabaisha nchi za kundi la G77+China kuchukua changamoto hizo kama somo na zisibweteke kusubiri msaada kutoka mataifa yaliyoendelea. 

Mkutano huo unaofanyika jijini Havana nchini Cuba tarehe 15-16 Septemba 2023 unakutanisha mataifa yanayoendelea unajadili changamoto zinazoikabili dunia baada ya kuathirika na janga la UVIKO-19 na migogoro inayoendelea duniani na vikwazo mbalimbali vya kiuchumi. 
Washiriki wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kundi la G77+ China wakifuatilia mkutano huo jijini Havana Cuba tarehe 15 Septemba 2023.

Mkutano huo umejikita kutafuta namna bora ya kujenga ustahimilivu kupitia maendeleo ya sayansi na teknolojia na ubunifu ili kundi la G77+China liweze kufikia malengo yake kwa pamoja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi katika picha ya pamoja na washiriki wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Kundi la G77+ China jijini Havana Cuba tarehe 15 Septemba 2023.

Mkutano huu utaongozwa na kaulimbiu isemayo “Changamoto za Maendeleo: Nafasi ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu”.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news