Rais Dkt.Samia ateuliwa GCA

DAR ES SALAAM-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan ameteuliwa rasmi kuwa Mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya Kituo cha Uhimilivu wa Mabadiliko ya Tabianchi (GCA).

Taarifa ya uteuzi huo imewasilishwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo na Katibu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa alipokutana na Rais Dkt.Samia pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika jijini Nairobi, Kenya.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Septemba 12, 2023 na Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus, uteuzi huo ni heshima ya utambuzi wa uongozi mahiri wa Rais Dkt.Samia.

Ni katika jitihada za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi Afrika na duniani kote ambapo Tanzania ni kinara kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali Afrika.

Wajumbe wengine wa Bodi hiyo ni Rais wa Senegal Macky Sail, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Moussa Mahamat, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Akinumwi Adesina na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Fedha Duniani (IMF), Kristalina Georgieva

GCA ni taasisi kubwa duniani inayosimamia masuala ya uhimilivu wa mabadiliko ya tabianchi ambapo hadi sasa imefanikisha upatikanaji wa zaidi ya dola za Marekani Bilioni 50 huku Tanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi za kwanza zitakazonufaika na fedha hizo katika kipindi cha miaka mitatu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news