Rais Dkt.Samia ziarani mkoani Lindi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza aliyewahi kuwa Mbunge wa Kilwa Kusini Suleiman Said Bungara Maarufu (Bwege) mara baada ya kuwahutubia Wananchi wa Kilwa Masoko Mkoani Lindi tarehe 19 Septemba, 2023. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mbunge wa Mchinga Mhe. Salma Kikwete mara baada ya kuwasili katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Lindi ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika Mikoa ya Kusini tarehe 19 Septemba, 2023. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Lindi ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika Mikoa ya Kusini tarehe 19 Septemba, 2023. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisikiliza maelezo ya Mtaalamu kutoka katika moja ya Vyumba vya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika Mikoa ya Kusini tarehe 19 Septemba, 2023. 
Wananchi wa Mkoa wa Lindi wakiwa kwenye Mkutano wa Hadhara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika eneo la Mitwero Mkoani Lindi ikiwa ni muendelezo wa ziara yake katika Mikoa ya Kusini tarehe 19 Septemba, 2023. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa pamoja na viongozi wengine wakati akivuta kitambaa kuweka jiwe la Msingi Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Lindi katika Kijiji cha Kilangala Mkoani humo tarehe 19 Septemba, 2023. 
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Lindi wakiimba Wimbo Maalum wakati wa mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Shuleni hapo katika Kijiji cha Kilangala hapo Mkoani Lindi tarehe 19 Septemba, 2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news