RC Dendego aguswa na Kitabu cha Madini yapatikanayo nchini, atoa wito GST

IRINGA-Mkuu wa Mkoa wa Iringa Halima Dendego amesema, mfumo unaotumiwa na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) wa kugawa Vitabu vya Madini yapatikanayo Tanzania kwa wakuu wa mikoa na wilaya,
Zoezi linaloenda sambamba na ufafanuzi wa masuala ya madini katika maeneo husika utasaidia mikoa husika kuondokana na uchimbaji wa madini wa kubahatisha bila kujua jiolojia ya maeneo hasa akitolea mfano Mkoa wa Iringa.

Dendego amesema hayo leo Septemba 17, 2023 Ofisini kwake mkoani Iringa baada ya kupokea Vitabu hivyo ambavyo ni nakala ya Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya za Iringa, Kilolo na Mufindi kutoka kwa Meneja wa Sehemu ya Jiolojia wa GST Maswi Solomon.
Aidha, Dendego ameipongeza GST kwa kuandaa kitabu hicho ambacho kikitumiwa vizuri kitakuwa mwarobaini kwa Wachimbaji Madini hususan kwa wale wanaochimba kwa kubahatisha sambamba na kuvutia uwekezaji hasa utafiti wa kina kwenye maeneo yaliyoainishwa na GST.

Pamoja na Mambo mengine, Dendego ametoa wito kwa GST kwa kuzingatia umuhimu wa kazi zake ni vyema kushiriki "Kongamano la Utalii Karibu Kusini" litakaloenda sambamba na maonesho mbalimbali ikiwemo Madini linalolenga kuifungua Mikoa ya Kusini na Nyanda za Juu Kusini hususan katika maana nzima ya Utalii.
"Naomba nichukue fursa hii kuwapongeza GST kwasababu mmekuja katika kipindi mwafaka, Mkoa wa Iringa umeandaa Kongamano la siku tano litakalo lenga kuifungua Mikoa ya Kusini na Nyanda za Juu Kusini, hivyo nawaomba sana GST mshiriki ili muweze kutusaidia kujibu maswali mbalimbali yatakayo ulizwa na Wawekezaji tuliowaalika," amesema Dendego.
Kwa upande wake, Meneja kutoka GST Maswi amesema ugawaji wa Vitabu hivyo kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya ni agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alilolitoa Jijini Mwanza katika Kongamano la Shirikisho la Wachimbaji Wadogo wa Madini (FEMATA) lililofanyika Jijini Mwanza.

Sambamba na hayo, Maswi amefafanua kuwa Mkoa wa Iringa unayo madini mkatati akitolea mfano Mbale za Bauxite zinazozalisha Alumina na Aluminium muhimu kwenye viwanda vya bidhaa za kimkakati ikiwemo vya teknolojia.
Aidha, Maswi amempongeza Mkuu wa Mkoa kwa kubuni Kongomano hilo la Utalii na kuona kwake umuhimu ya GST kushiriki kwani mkoa wa Iringa unazo fursa za utalii wa jiolojia.

Ni kutokatana na mabadaliko ya jiolojia kwenye maeneo ya mkoa huo akitolea mfano Isimila Natural Stone Pillars ambazo pia zilitajwa kwenye kitabu hicho.
Aidha, ameahidi GST itatoa ushirikiano wa kuibui na kutangaza vivutio hivyo kwani ni chanzo kingine cha mapato ya ndani pamoja na kujipatia fedha za kigeni.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news