Rushwa haitakuwa na nafasi-Waziri Bashungwa

DODOMA-Waziri wa Ujenzi, Mhe. Innocent L. Bashungwa(Mb) amemshukuru Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumuamini na ameahidi kudhibiti na kupambana na rushwa katika mikataba, manunuzi na usimamizi wa miradi.
Amesema hayo leo tarehe 06 Septemba 2023 Bugeni Dodoma wakati alipopata nafasi ya kujibu maswali ya Waheshimiwa Wabunge Kwa mara ya kwanza tangu alipoteuliwa na Kuapishwa na kuwa Waziri wa Ujenzi.

“Ninamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuendelea kuniamini, Mimi pamoja na Niabu Waziri tunamhadi kufanya kazi kwa bidii kwa kupambana na kudhibiti Rushwa hasa kwenye maeneo ya mikataba, manunuzi na usimamizi wa miradi, ili dhamira ya Mheshimiwa Rais na Utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi uende Vyema”

Aidha, Wakati akijibu Swali la nyongeza la Mbunge wa Jimbo la Tandahimba, Mhe. Katani Ahmed aliyetaka kujua lini Serikali itatenga fedha ya dharura kujenga kipande cha Barabara ya Nguja - Mkwiti - Tandahimba yenye maeneo Korofi.

Bashungwa amewaigiza Maneneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mikoa yote kufanya Upembuzi yakinifu na kubaini maeneo yote korofi ya Barabara na kuyawasilisha Wizarani ili yaweze kupewa kipaumbele wakati wa kuandaa bajeti.

“Nitumie nafasi hii kuwaelekeza Mameneja wa TANROADS mikoa yote kuangalia maeneo yote korofi na kufanya Upembuzi yakinifu na kuyawasilisha Wiazarani ili yapewe kipaumbele wakati wa kuandaa bajeti” amesema Bashungwa

Kadhalika, Mbunge wa Tandahimba, Mhe. Katani Ahmed alitaka kujua Je, ni lini ujenzi wa kiwango cha lami wa barabara kutoka Mtwara – Nanyamba – Tandahimba – Newala hadi Masasi utaanza, ambayo ipo kwenye Ilani ya Uchaguzi 2020 na ahadi ya Mheshimiwa Rais.

Wakati akijibu swali hilo, Bashungwa amesema ujenzi wa barabara ya Mtwara – Nanyamba – Tandahimba – Newala – Masasi yenye urefu wa kilometa 210 unatekelezwa kwa awamu ambapo ujenzi kwa kiwango cha lami wa sehemu ya Mtwara – Mnivata (km 50) umekamilika kwa kutumia fedha za ndani.

Bashungwa amesema kuwa sehemu ya barabara ya Mnivata – Newala - Masasi (km 160) chini ya ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imesainiwa tarehe 21 Juni, 2023 kwa sehemu za Mnivata – Mitesa (km 100) na Mitesa – Masasi (km 60) pamoja na ujenzi wa Daraja la Mwiti, kwa sasa Makandarasi wa sehemu zote mbili wapo katika hatua za maandalizi ya kuanza ujenzi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news