Singida Fountain Gate yaichapa Future FC bao 1-0

DAR ES SALAAM-Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kimataifa kupitia Kombe la Shirikisho barani Afrika,Singida Fountain Gate imeibuka na ushindi wa bao 1-0.

Ni baada ya kucheza kandanda safi dhidi ya Future FC ya Misri katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mwisho ya kuwania kuingia hatua ya makundi ya kombe hilo.

Septemba 17, 2023 mshambuliaji mpya kutoka nchini Kenya, Elvis Rupia aliweza kubadilisha mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex uliopo Kata ya Chamanzi ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Rupia amejiunga na klabu yake mpya siku chache zilizopita na tayari amefanya matokeo chanya kwenye mechi yake ya kwanza.

Matokeo hayo ya uhakika yanawapa wawakilishi hao katika Kombe la Shirikisho fursa ya kufuzu katika hatua ya makundi ya mchujo.

Hata hivyo,vijana hao wanatarajia kusafiri hadi Cairo, Misri kwa mchezo wa marudiano ambao mshindi wake wa jumla atatinga hatua ya 16 bora.

Aidha, kabla ya kusafiri kwenda Misri,timu hiyo yenye maskani yake mkoani Singida itacheza na Azam FC katika mechi ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news