Tanzania, Afrika Kusini zakubaliana Sekta ya Afya

JOHANNESBURG-Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Afrika Kusini zimeingia makubaliano ya ushirikiano katika Sekta ya Afya baina ya nchi hizo mbili ili kuweza kuboresha zaidi huduma za afya na ushirikiano wa pamoja katika kubadilishana uzoefu na watalaam wa Afya.
Makubaliano hayo yamefanyika Septemba 1, 2023 kupitia Waziri wa Afya Tanzania Mhe. Ummy Mwalimu na Waziri wa Afya Afrika Kusini Mhe. Dkt. Mathume Joseph Phaahla Jijini Johannesburg, Afrika Kusini ambapo Viongozi hao wamekubaliana kuwa na mpango wa utekelezaji na ufuatiliaji wa mkataba huo na kutoa taarifa kila mwaka.
“Tanzania na Afrika Kusini zimekuwa na ushirikiano wa muda katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya Afya, kusainiwa kwa hati hii kutachangia kuboresha ushirikiano katika sekta ya Afya ikiwemo kubadilishana wataalam wabobezi kwenye fani mbalimbali za afya. 

"Kuwezesha mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu na kubadilishana teknolojia, kuboresha upatikanaji wa dawa, chanjo na udhibiti wa magonjwa ya mlipuko pamoja na dharura za Afya,”amesema Waziri Ummy na kuongeza kuwa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili utaimarisha mfumo wa huduma za rufaa kwa wagonjwa watakaohitaji matibabu nchini Afrika Kusini.
“Kusainiwa kwa hati hii moja ya maazimio ya Mkutano wa Pili wa mataifa mawili( Bi - National Commission - BNC) baina ya Tanzania na Afrika kusini ambapo Azimio Na. 43 lilielekeza kwamba, Hati ya Makubaliano katika sekta ya Afya isainiwe baada ya taratibu zote ambapo Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe Cyril Ramaphosa, Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini walisisitiza umuhimu wa kutekeleza maafikiano yaliyofikiwa na kutoa mrejesho wa utekelezaji kwa wakati” amefafanua Mhe. Ummy.

Kwa upande wake Mhe.Dkt. Phaahla, Waziri wa Afya wa Afrika Kusini amepongeza hatua ya kusainiwa kwa hati ya makubaliano haya ambayo imefanyika katika kipindi ambacho nchi za Dunia nzima na Bara la Afrika zikiwemo nchi za Afrika Kusini na Tanzania zinakabiliwa na majanga mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya tabia nchi inayopelekea milipuko ya magonjwa na ukosefu wa vyakula.
Utiaji saini wa makubaliano haya ni utaimarisha zaidi ushirikiano katika masuala yaliyoanzishwa kama vituo vya kudhibiti na kuzuia magonjwa, wakala wa dawa, mifumo ya ununuzi wa pamoja wa dawa,” ameeleza Mhe. Dkt. Phaahla.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news