Tanzania yakabidhiwa Urais wa Mtandao wa Jiopaki barani Afrika

NA KASSIM NYAKI
NCAA

JAMHURI ya Muungano wa Tanzania kupitia Jiopaki pekee iliyoko Kusini mwa Jangwa la Sahara ya Ngorongoro-Lengai, ambayo inatambuliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) imekabidhiwa Urais wa mtandao huo katika kikao cha 10 cha Kidunia cha UNESCO Jiopaki kinachofanyika katika mji wa Marrakesh nchini Morocco.
Ujumbe kutoka Tanzania ulioko nchini Morocco kupokea heshima hiyo umeongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Jenerali Venance Mabeyo (mstaafu), Kamishna wa Uhifadhi wa NCAA, Dkt. Freddy Manongi.

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi Mhandisi Joshua Mwankunda (kushoto) akikabidhiwa cheti cha kuwa Rais wa Mtandao wa Jiopaki Barani Afrika kutoka kwa Rais anayemaliza muda wake, Bw.Driss Achbal kutoka nchini Morocco katika vikao vinavyoendelea nchini Morocco kuanzia Septemba 9, 2023

Rais Mpya wa Mtandao wa Jiopaki Afrika aliyechaguliwa ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Mhandisi Joshua Moshi Mwankunda ambaye ni Meneja wa Idara ya Urithi wa Utamaduni na Jiolojia NCAA.
Faida kubwa ambazo nchi ya Tanzania itazipata kupitia uongozi wa mtandao huo ni pamoja na;

1. Kuongezeka kwa muonekano chanya wa nchi ya Tanzania kimataifa,

2. Kuongezeka kwa idadi ya watalii na watafiti watakaotembelea nchi ya Tanzania kwa Shughuli mbalimbali.

3. Kupanua wigo wa mashirikiano ya kimataifa katika sekta ya uhifadhi na utalii wa jiopaki na miamba (Geopark)

4. Fursa ya kuongeza vivutio vingi vya utalii wa miamba kupitia uanzishwaji wa jioapaki mpya nchini Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news