Ubunifu wa Prof.Muhongo wakoleza kasi ya elimu jimboni

NA FRESHA KINASA

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof. Sospeter Muhongo ameendesha harambee kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Rukuba.
Kupitia harambee hiyo, Mheshimiwa Prof.Muhongo ametoa mifuko 200 ya saruji pamoja na fedha huku viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya hiyo, Serikali, walimu makada pamoja na wananchi wakishiriki kuchangia ujenzi wa shule hiyo.

Harambee hiyo imefanyika Septemba 27,2023, ambapo Kisiwa cha Rukuba ni moja ya vijiji vinne vya Kata ya Etaro na wanafunzi wa sekondari kutoka kisiwani humo wanasoma nchi kavu kwenye sekondari ya kata yao ya Etaro Sekondari.

Wananchi wa Kisiwa cha Rukuba wamesema, ujenzi wa shule hiyo utakuwa na matokeo chanya kwani utasaidia watoto kusoma na kuhitimu masomo yao na kuondokana na changamoto ya kuvushwa kwenda masomoni. Hali ambayo inapelekea baadhi yao kukatisha masomo.

Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dkt.Halfan Haule amesema kuwa,Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za wananchi hao katika kuhakikisha ujenzi wa shule hiyo unakamilika.

Katika taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini leo Septemba 30, 2023 imebainisha kuwa, "Wanafunzi hao wanakumbuna na matatizo mengi mno ambayo yanadhoofisha sana maendeleo yao kielimu.

"Kwa hiyo, wakazi wa Kisiwa cha Rukuba wameamua kujenga sekondari yao kisiwani humo.Harambee yenye mafanikio makubwa iliyoendeshwa na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini siku ya Jumatano ya Septemba 27,2023 ilishirikisha viongozi wote Mkuu wa Wilaya ya Musoma na halmashauri yake (Musoma DC)."

"Wafanyakazi wa kada mbalimbali, wakiwemo walimu, Makada ya CCM walishiriki. Kamati ya Siasa ya Wilaya CCM nayo ilishiriki na ilikuwa ni harambee ya kipekee kufanyika kisiwani humo."

MICHANGO ILIYOPATIKANA KWENYE HARAMBEE HIYO.

Wakazi na Wazaliwa wa Kisiwa cha Rukuba:

Saruji Mifuko 167,

Kamati ya Siasa ya Kata (CCM):

Saruji Mifuko 22,

Kamati ya Siasa ya Wilaya (CCM):

Saruji Mifuko 15,

DED na wenzake -Saruji Mifuko 20,

DC na wenzake- Saruji Mifuko 62,

Mbunge wa Jimbo: Saruji Mifuko 200,

Fedha taslimu: Tsh 248,000 zikiwemo shilingi 105,000 za walimu na Makada wa CCM. "Karibuni tujenge Sekondari ya Kisiwa cha Rukuba cha Musoma Vijijini." imeeleza taarifa hiyo."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news