Yanga SC yaichapa El Marreikh mabao 2-0

KIGALI-Mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania, Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam imeichapa Klabu ya El Marreikh ya Sudan mabao 2-0 katika michuano ya hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa barani Afrika.

Ni kupitia mtanange wa kuvutia amabo umepigwa Septemba 16, 2023 katika Dimba la Pele lililopo jijini Kigali nchini Rwanda.

Wawakilishi hao wa Tanzania katika michuano ya Kimataifa walionekana wakicheza kwa kujiamini kama ipo nyumbani.

Vile vile, klabu hiyo ambayo kwa siku za karibuni imeonekana kuwa moto, ilikosa magoli mengi kipindi cha kwanza hali iliyofanya mpaka timu hizo zinakwenda mapumziko, ubao ulisoma pande zote sufuri.

Kennedy Musonda aliwainua mashabiki wa Yanga SC kwa kukwamisha wavuni mpira kwa kichwa dakika ya 60 akiwa katikati ya ulinzi mkali wa mabeki wa Klabu ya El Marreikh ya Sudan.

Wakari huo huo,Clement Mzize kupitia mchezo huo wa kwanza wa Hatua ya 32 Bora ndani ya dakika ya 78 alipiga msumari wa mwisho.

Ni baada ya kuitumia vema pasi ya mwisho aliyotengewa na midfielder Stephane Aziz Ki kwenye 18 ya Klabu ya El Marreikh ya Sudan.

Aidha, El Merreikh ya Sudan wamelazimika kutumia Uwanja wa Pele kama wa nyumbani kutokana na machafuko yanayoendelea nchini Sudan.

Jumamosi ijayo, wababe hao wa soka Afrika watarudiana jijini Dar es Salaam na mshindi wa jumla atakwenda hatua ya 16 bora ambayo itachezwa kwa mfumo wa makundi kulingana na ratiba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news