Clatous Chama aifuta machozi Simba SC mbele ya Power Dynamos

NDOLA-Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam imetoa sare ya kufungana mabao 2-2 na wenyeji Power Dynamos ya nchini Zambia.

Ni katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 32 bora Ligi ya Mabingwa barani Afrika ambao umepigwa Septemba 16, 2023 katika Dimba la Levy Mwanawasa lililopo Ndola,Zambia.

Licha ya Simba SC kuonekana wakiwa makini kila dakika waliruhusu goli la kwanza kutoka kwa wapinzani wao. Mpaka timu hizo zinakwenda mapumziko,wageni hao walikuwa nyuma kwa goli moja.

Joshua Mutale aliifungia Power Dynamos bao la kuongoza katika dakika ya 29 hali iliyopelekea mashabiki wa nyumbani kushangilia.

Baada ya mapumziko, winga wa zamani wa Power Dynamos, Clatous Chota Chama ‘Triple C’ alifuta bao la kwanza la Mutale dakika ya 59.

Aidha,Cephas Mulombwa dakika ya 74 alirejesha bao kwa Power Dynamos ambalo lilionekana kuwa,kikwazo hadi pale ambapo Clatous Chota Chama alirejea tena dakika 90 na kubadili furaha ya wenyeji hao.

Hata hivyo,hadi refa anapuliza kipenga cha mwisho, timu hizo zilitoshana nguvu kwa magoli 2-2 huku miamba hiyo ya soka barani Afrika ikitarajiwa kurudiana Jumapili ijayo jijini Dar es Salaam.

Matokeo ya mtanange huo jijini Dar es Salaam, yatatoa majibu ni nani atakwenda hatua ya 16 bora ambayo itachezwa kwa mfumo wa makundi kulingana na ratiba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news