Askari wa Jeshi la Polisi ajipiga risasi kisa wivu wa mapenzi

MBEYA-Askari wa Jeshi la Polisi mwenye namba J.2596 Konstebo Samwel Feston Kaziyote mwenye miaka 24 amejiua kwa kujipiga risasi kutokana na kile kilichoelezwa kuwepo kwa mzozo baina yake na mpenzi wake.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga kituo cha kazi cha askari huyo aliyejiua kilikuwa kituo kikuu cha Polisi Mbeya.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda Kuzaga kwa vyombo vya habari imeeleza kuwa, tukio hilo lilitokea Oktoba 2, 2023 majira ya saa mbili na robo usiku maeneo ya Mtaa wa Mzumbe uliopo Forest ya zamani jijini Mbeya.

Kamanda Kuzaga amesema, majira hayo ya usiku akiwa kazini askari huyo aliacha lindo la benki na kwenda nyumbani kwa mpenzi wake maeneo ya Mzumbe ambako alijipiga risasi kidevuni na kusababisha kifo chake papo hapo.

“Uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni mzozo uliotokea baina yake na mpenzi wake baada ya marehemu kuacha lindo la Benki na kisha kuondoka na silaha bunduki kwenda nyumbani kwa mpenzi wake huyo na kujipiga risasi.”

Kamanda huyo amesema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi zaidi kuhusiana na tukio hilo ili hatua zaidi ziweze kuchukuliwa ambapo tayari mpenzi wa marehemu mwenye umri wa miaka 30 ambaye majina yake yamehifadhiwa anashikiliwa kwa mahojiano.

Hata hivyo taarifa hiyo ya Kamanda Kuzaga haikuweka bayana iwapo baada ya askari huyo kufika nyumbani kwa mpenzi wake kulikuwa mazungumzo yoyote yaliyofanyika baina ya wapenzi hao kabla hajachukua uamuzi wa kujitoa uhai wake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news