Baraza la Michezo la Taifa lapewa kongole

DODOMA-Kamati ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo chini ya Mwenyekiti Mhe. Husna Sekiboko imelipongeza Baraza la Michezo la Taifa kwa kuendelea kusimamia Sekta ya Michezo ambayo kwa sasa inaitangaza vyema Tanzania na kusimamia Utawala Bora ambao umepunguza migogoro katika sekta hiyo.
Pongezi hizo zimetolewa baada ya kuwasilishwa kwa Taarifa ya Utekekezaji wa Majukumu ya Baraza hilo Oktoba 25, 2023 jijini Dodoma, iliyowasilishwa na Bi. Neema Msitha kwa niaba ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro.

Akiwasilisha taarifa hiyo, Bi. Neema Msitha amesemaSekta hiyo imeendelea kupata mafanikio makubwa ikiwemo kuwa mwenyeji wa Mashindano ya AFCON mwaka 2027, kuanzishwa kwa Mfuko wa Maendeleo ya Michezo ambao umesaidia Timu za Taifa katika mashindano mbalimbali.

"BMT imefanikiwa kuanzisha mfumo wa Kidigitali, Usajili wa Vyama na Mashirikisho, na Michezo mbalimbali ikiwemo Riadha, Timu za Mpira wa Miguu, Netiboli, Gofu, Ngumi zimefaidika na Mfuko wa Maendeleo ya Michezo," amesisitiza Bi. Neema Msitha.

Kwa upande wake Mwenyekiti huyo, Mhe. Husna Sekiboko ameielekeza Wizara iangalienamna bora ya kusimiamia vyema Idara zinazosimamia Maendeleo ya Michezokatika ngazi ya Mikoa na Halmashauri pamoja nakuhakikisha mtiririko wa asilimia tano za michezo ya kubahatisha inafika kwa wakati.

Wakichangia taarifa hiyo Wajumbe wa Kamatiwamepongeza uhusiano uliopo kati ya Wizara inayosimamia michezo Tanzania Bara na Zanzibar, huku wakishaurikuajiri walimuwa michezo, kufanyika mashindano mbalimbali ikiwemo Taifa Cup pamoja na kuhakikisha asilimia tano ya michezo ya kubahatisha inafanya kazi yake ipasavyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news