Dkt.Mpango akabidhi hatimiliki za kimila Makete

NA MUNIR SHEMWETA
WANMM

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Philip Isdori Mpango amekabithi Hati ya Hakimiliki za Kimila kwa wananchi wa Wilaya ya Makete Mkoa wa Njombe.

Makamu wa Rais Mhe. Dkt Philip Isdori Mpango akikabidhi Hatimiliki za Kimila kwa wananchi wa Makete mkoa wa Njombe wakati wa ziara yake ya siku tatu mkoani humo tarehe 27 Oktoba 2023. Katikati ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda.

Dkt. Mpango amekabidthi hati saba za mfano kati ya Hatimiliki za Kimila 6,883 zilizoandaliwa Oktoba 27,2023 katika hafla iliyofanyika Kijiji cha Tandala Wilayani humo akiwa katika ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoa wa Njombe.
Akizungumza mbele ya Makamu wa Rais, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geofrey Pinda amesema, utolewaji Hati za Kimila wilayani Makete unafuatia uwezeshwaji uandaaji mipango ya matumizi bora ya ardhi uliofanywa na wizara yake kupitia Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi katika vijiji.
Kwa mujibu wa Mhe. Pinda mkoa wa Njombe una jumla ya vijiji 323 ambapo vijiji 264 kati ya hivyo tayari vimewezeshwa kuandaliwa mpango wa matumizi bora ya ardhi.

"Mhe Makamu wa Rais mkoa wa Njombe tunavyo vijiji 323 na kati ya hivyo vijiji 295 tayari vimewezeshwa na sasa tuko katika wilaya ya Makete kama taarifa ilivyoeleza," alisema Mhe. Pinda.


Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete, Bw. William Makufwe amesema kuwa, upatikanaji wa Hatimiliki hizo ni jitihada za Wilaya kukuza zao la ngano àlilolieleza kuwa linazalishwa kwa wingi katika Wilaya hiyo.
Aidha, Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa, Wilaya yake imeamua kuendesha kilimo cha zao hilo Kimkakati kwa kupima na kumilisha mashamba kupitia Hatimiliki za Kimila ili ziwape fursa wakulima ya kuongeza mitaji itakayoinua wigo wa uzalishaji zao hilo.

Ugawaji wa Hatimiliki hizo unafuatia kazi iliyofanywa na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupitia Tume ya Taifa ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi iliyowezesha uandaaji wa Mipango ya Matumizi ya Ardhi ya Vijiji 64 katika wilaya ya Makete na kutoa jumla ya Hatimiliki za Kimila 6,889.


Makamu wa Rais Mhe. Dkt Philip Isdori Mpango akiwa katika picha ya pamoja na wananchi aliowakabidhi Hatimiliki za Kimila katika wilaya ya Makete mkoa wa Njombe wakati wa ziara yake ya siku tatu mkoani humo tarehe 27 Oktoba 2023.

Kazi hiyo imetekelezwa katika awamu mbili ambapo, wamu ya kwanza, ilihusisha uandaaji mipango ya matumizi ya ardhi katika vijiji 44 na upimaji wa vipande vya ardhi katika vijiji 17 ambapo jumla ya hati 6,594 ziliandaliwa.


Makamu wa Rais Mhe. Dkt.Philip Isdori Mpango akisoma kitabu cha Mpango wa Matumizi Bora ya Ardhi alipotembelea banda la Halmashauri ya wilaya ya Makete wakati wa ziara yake ya siku tatu mkoani humo tarehe 27 Oktoba 2023. Kulia ni Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Geofrey Pinda. (PICHA ZOTE NA WIZARA YA ARDHI).

Aidha, katika awamu ya pili uandaaji wa mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji 20 kwenye Tarafa ya Ukwama na Lupalilo ulifanyika ambapo Vijiji 20 viliwezeshwa kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi na hati miliki za kimila 287.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news