Hamas warusha makombora Mji wa Sderot nchini Israel

SDEROT-Mji wa Sderot uliopo Kusini mwa Israel umewekwa chini ya tahadhari nyekundu leo Jumamosi asubuhi baada ya Hamas kurusha makombora kwenye mji huo.
Picha iliyopigwa kutoka mji wa Israel wa Sderot inaonesha moshi mweusi ukipanda kutoka Gaza leo Oktoba 14, 2023. (Picha na Thomas Coex/AFP/Getty Images).

Sderot ni mji wa Magharibi karibu na Jiji la Negev. Mwaka 2021, ulikuwa na idadi ya watu 30,553 ambapo Sderot iko karibu na Gaza, na sehemu ya karibu zaidi ikiwa umbali wa mita 840.

Katika chapisho kwenye Telegram leo Jumamosi,vikosi vya Hamas vya al-Qassam vilisema vimerusha roketi katika mji huo wa Sderot.

Aidha, timu ya CNN huko Sderot ilisikia mfumo wa ulinzi wa anga wa Iron Dome wa Israel ukifanya kazi kuzuia roketi. Mwanatimu mmoja alisikia king'ora kikionesha kwamba jiji lilikuwa chini ya tahadhari.(Agencies)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news