Vifaa tiba, dawa kwa ajli ya kuisaidia Gaza vyawasili Misri

CAIRO-Vifaa tiba na dawa kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa ajili ya kusaidia Gaza vimetua Misri karibu na kivuko cha Rafah, kulingana na Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus.

Licha ya vifaa hivyo kuwasili salama nchini Misri, bado havijatumwa kwenda Gaza kwani, shirika hilo linaangalia namna ya sahihi ya ufikiaji wa kibinadamu kupitia njia ya kuvuka.

"Ni ombi letu kwa Israel kufikiria upya uamuzi wa kuwahamisha watu milioni 1.1. Litakuwa janga la kibinadamu,"ameeleza Mkurugenzi Mkuu wa WHO.

Aidha, baada ya mashambulizi ya Hamas, Israel ilifunga vivuko vyake viwili vya mpaka na Gaza na kuzingira eneo hilo, kuzuia usambazaji wa mafuta, umeme na maji.

Uamuzi huo umeacha kivuko cha Rafah kati ya Gaza na Misri kama njia pekee inayoweza kuwatoa watu kutoka katika eneo hilo na vifaa kuingia humo. Lakini haijulikani ikiwa hata kuvuka inawezekana.

Vile vile, upande wa Misri wa kivuko uko wazi, lakini upande wa Palestina haufanyi kazi kufuatia mashambulizi mengi ya anga ya Israel mapema wiki hii, afisa mkuu wa Jordan aliiambia CNN Alhamisi.

"Wa-Jordan na Wamisri wanasubiri kibali cha usalama kutoka kwa Waisraeli ili kuruhusu (msaada) malori kuvuka bila tishio la mashambulizi mengine ya anga.”

Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri siku ya Alhamisi ilikanusha ripoti za kufungwa kwa kivuko hicho, ikisema kimepata uharibifu kutokana na mashambulizi ya anga ya mara kwa mara ya Israel upande wa Palestina.

Hata hivyo, CNN haikuweza kuthibitisha ikiwa kivuko kimefunguliwa, ingawa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken alisema Jumatano kwamba utawala wa Biden uko kwenye mazungumzo na Israel na Misri kuhusu kuunda njia ya kibinadamu ambayo raia wanaweza kupita. (Agencies)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news