Job, Aziz Ki na Max wa kwanza kuwania Tuzo ya NIC Insurance

DAR ES SALAAM-Dickson Nickson Job,Stephane Aziz Ki na Max Mpia Nzengeli wanachuana kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora katika Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Saalam.

Kupitia tuzo hiyo ya mwezi Oktoba,mwaka huu inakuwa ya kwanza baada ya klabu hiyo kuingia mkataba na Shirika la Bima la Taifa (NIC).

Ushirikiano huo kati ya Shirika la Bima la Taifa na Klabu ya Yanga utadumu kwa miaka mitatu, kuanzia msimu huu wa 2023 mpaka 2026.

Ushirikiano huo unazikutanisha taasisi mbili zenye historia kubwa ya ufanisi na weledi Tanzania ambapo NIC Insurance ni kampuni ya serikali ikiwa na uzoefu wa miaka 60 ya utoaji wa huduma mbalimbali za bima kwa Watanzania wakati Yanga ni klabu kongwe na mabingwa wa kihistoria katika mpira wa miguu nchini.

Dhumuni kuu la NIC Insurance kuamua kuingia ushirikiano huo ni kuunga mkono vilabu vya ndani kama Yanga pamoja na sekta nzima ya michezo.

"Tunaamini kuwa ushirikiano huu utaleta chachu kwa wachezaji wa Yanga kujituma zaidi na kuonyesha ubora wao kwa timu na kila mechi kuisaidia timu yao huku mwisho wa mwezi wakiwa na uhakikwa wa kupata zawadi kutoka kwetu.

“Huwezi kuzungumzia bima bila kuitaja NIC, na katika soka Yanga ni nembo ya soka kwa Tanzania akiwa bingwa wa kihistoria. Tunayo furaha kubwa kupata fursa ya kufanya biashara na taasisi kubwa kama hii. Kwa upande wetu NIC imepewa hadhi ya kuaminika,"amesema Dkt.Elihuruma Doriye ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa NIC Insurance.

Aidha, tuzo hizo ambazo zinaanza mwezi huu, Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa NIC Insurance, Karim Meshack amesema, mshindi wa tuzo hiyo atazawadiwa fedha taslimu shilingi milioni nne.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news