Ninaungana na Mheshimia Rais Dkt.Samia kukupongeza sana Dkt.Tulia-Waziri Mkuu

NA GODFREY NNKO

WAZIRI Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa ameungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan kumpongeza Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa 31 wa Umoja wa Mabunge ya Duniani (IPU).

"Ninaungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kukupongeza kwa dhati Dkt.Tulia Ackson, Mbunge wa Mbeya Mjini na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuaminiwa na kuchaguliwa kuwa Rais wa 31 wa Umoja wa Mabunge ya Dunia-IPU;

Mheshimiwa Majaliwa ametoa pongezi hizo Oktoba 27,2023 saa chache baada ya Dkt.Tulia kutangazwa mshindi wa kiti hicho.

"Ushindi huu ni kielelezo cha imani kubwa ambayo mataifa mengi duniani wanayo juu ya nchi yetu na wewe mwenyewe.Ninakutakia kheri katika jukumu hili linalounganisha Mataifa yetu pamoja ili kujadili mwelekeo chanya wa Dunia.Hongera sana kwa ushindi,"amebainisha Mheshimiwa Waziri Mkuu.

Awali Spika wa Bunge la Tanzania Dkt.Tulia Ackson alishinda kwa kishindo kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) kupitia uchaguzi uliofanyika Oktoba 27,2023 jijini Luanda nchini Angola.

Mhe. Dkt Tulia ameshinda uchaguzi huo mara baada ya kupata kura 172 ambazo ni sawa na asilimia 57 ya kura 303 zilizopigwa na Wajumbe walioshiriki Mkutano wa 147 wa IPU.

Dkt.Tulia amewashinda wagombea wengine watatu waliogombea nafasi hiyo ambao ni Mhe. Adji Diarra kutoka Bunge la Senegal aliyepata kura 59, Mhe. Catherine Hara Spika wa Bunge la Malawi aliyepata kura 61 na Mhe. Marwa Hagi kutoka Bunge la Somalia aliyepata kura 11.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news