Msigwa afungua rasmi Tamasha la 42 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo

PWANI-Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Bw. Gerson Msigwa amefungua rasmi Tamasha la 42 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo lililohudhuriwa na wananchi na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi akieleza kuwa Utamaduni na Sanaa ni Sekta zenye umuhimu mkubwa katika kuleta maendeleo na kukuza ajira hapa nchini.

Katibu Mkuu Bw. Msigwa amesema hayo usiku wa Oktoba 26, 2023 wakati akifungua rasmi tamasha hilo linaloendelea katika viwanja vya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa).

"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatambua kwamba eneo la Sanaa katika nchi yetu ni la kimkakati, ni lazima tulitumie kimkakati. Naomba sana vijana wenye vipaji wasizuiliwe kufanya Sanaa, huku nako kuna ajira," amesisitiza Katibu Mkuu Bw. Msigwa.

Hafla ya ufunguzi wa Tamasha hilo ambalo linafanyika kwa siku tatu kuanzia Oktoba 26 - 28, 2023 katika Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBA) limehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mwenyekiti wa Bodi ya taasisi hiyo Bw. George Yambesi, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa Dkt. Emmanuel Ishengoma, viongozi na wakazi wa Wilaya ya Bagamoyo.

Baadhi ya Wasanii na vikundi vilivyofungua tamasha hilo ni pamoja na:Wamwiduka Band, Worrious from the East, msanii Vitalis Maembe, na wengine wengi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news