Rais Dkt.Mwinyi awaombea dua njema wananchi mbalimbali

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhajj Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameendeleza utaratibu wake wa kuwajuulia hali wazee na wananchi kwenye maeneo mbambali kwa kuwaombea dua na kuwatakia kheir na shufaa wagonjwa wapone haraka kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu.

Alhaj Dkt.Mwinyi amewatembelea Haji Ramadhan Suweid Buda, mwandishi wa
habari mkongwe na mama mzazi wa Sheikh Samir Zulfikar wa Mahad el Juneid ya
Mkunazini ambao wanaendelea na matibabu Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja.

Pia, Alhaj Dkt.Mwinyi aliwatembelea wazee wa Chama Cha Mapinduzi ambao walitoa
mchango mkubwa kwenye chama hicho akiwemo Kombo Mzee Kombo nyumbani kwake Miembeni Mkoa wa mjini Magharibi,Bw.Bora Afya Silima Haji nyumbani aliyekua Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Kichama nyumbani kwake Mwembelikunda na Bi.Hiari Miraji Othman, Balozi wa nyumba 10 namba mbili huko nyumbani kwake Miembeni Jitini.

Mapema, Alhaj Rais Dkt.Mwinyi alijumuika na waumini wa dini ya Kiislam na wananchi wa Miembeni kwenye ibada ya sala ya Ijumaa kwenye msikiti wa Ijumaa,Miembeni, Wilaya ya Mjini.

Akizungumza kwenye ibada hiyo Katibu Mtendaji kutoka Ofisi ya Mufti Zanzibar,Sheikh Khalid Ali Mfaume aliwahimiza waumini wa Kiislam umuhimu wa tabia njema na kueleza kuwa tabia njema ni msingi wa mambo manne ikiwemo imani.

Sheikh Khalid alieleza kwenye tabia njema imani hudumu kwa kutekelezwa amri za Allah (S.W) pamoja na kufuatwa makatazo yake. Pia alieleza kukosekana kwa tabia njema imani hupungua na kuongezeka kwa vitendo vya kuporomoka kwa maadili ikiwemo kupungua kwa heshima kwenye familia na jamii.

Alisema siku hizi watoto hawawaheshimu wakubwa zao wakiwemo wazazi na walezi hata jamii zinazowazunguruka, aliiasa jamii ili kupunguza wimbi la ukosefu wa maadili na kuepusha athari kubwa za ndoa na takala zinazojitokeza kwenye jamii ni vyema kutafuta njia za busara ili kukinusuru kizazi cha sasa kilichogubigwa na wimbi la ukosefu wa heshima na maadili.

Pia aliiasa jamii kuendelea kuwafundisha mema watoto ili kukuza jamii yenye heshima na maadili mema na tabia njema.

Kwa upande wake, Khatib wa ibada hiyo ya sala ya Ijumaa aliiasa jamii kwamba uzuri wa waumini na waislam ni elimu, adabu na kuheshimu viongozi na jamii inayowazunguruka kwa kujiepuka kutoa maneno yasiyofaa kwa viongozi, wazazi na jamii ili kujenga jamii iliyonjema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news