Rais Dkt.Samia aanza ziara ya kikazi mkoani Singida

SINGIDA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema serikali itaendelea kuhakikisha huduma ya elimu inasogezwa karibu na wananachi ili kuondoa adha ya wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata elimu.

Rais Samia amesema hayo leo wakati akihutubia wananchi katika eneo la uwanja wa
Police Square wilayani Manyoni ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi
mkoani Singida.

Rais Samia amesema kupitia mradi wa Kuimarisha Elimu ya Awali na Msingi nchini
(BOOST) na Mradi wa Kuimarisha Elimu ya Sekondari (SEQUIP) serikali inajenga
shule za msingi na sekondari katika mikoa yote nchini.

Rais Samia amesema lengo la miradi hiyo ni kuondoa msongamano katika madarasa
ili kuongeza tija na ufanisi kwenye ufundishaji kutoka wanafunzi 120 kwa darasa hadi kufikia 45.

Awali Rais Samia alifungua Shule ya Msingi Imbele yenye thamani ya shilingi milioni
493.4 na mabweni ya madarasa ya Shule ya Sekondari Mwanamwema Shein katika
Manispaa ya Singida.

Rais Samia pia aliweka Jiwe la Msingi, ujenzi wa barabara ya Mkiwa - Itigi - Noranga
(56.9km) kwa kiwango cha lami yenye thamani ya shilingi bilioni 67.2 bilioni ambayo
ni sehemu ya barabara ya Makongorosi- Rungwa – Itigi – Mkiwa (413km).

Barabara hii licha ya kuunganisha ushoroba wa Tanzania na Zambia pamoja na wa
kati itaunganisha pia Tanzania na ukanda wa SADC na hivyo kuchochea shughuli za
uzalishaji na biashara kwa kurahisisha usafiri na usafirisha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news