Huduma ya kuweka Puto sasa inapatikana Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila na Upanga

DAR ES SALAAM-Baada ya kuimarisha huduma mbalimbali ikiwemo kuweka puto Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa watu wanaopenda kupungua uzito sasa huduma hii pia imeanza kutolewa MNH-Upanga.
Hayo yamezungumzwa na Daktari Bingwa Mbobezi wa Upasuaji Mfumo wa Chakula, Ini na Mbobezi wa Upasuaji Kutumia Matundu Madogo MNH, Dkt. Kitembo Salum Kibwana na kusisitiza kuwa lengo ni kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma hiyo.

Dkt. Kitembo amesema kuwa mwishoni mwa wiki hii tayari mtu mmoja amepata huduma hiyo MNH-Upanga ambapo MNH-Mloganzila watu 150 wameishahudumiwa tangu kuanzishwa kwa huduma hiyo mwishoni mwa mwaka jana 2022.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news