Rais Dkt.Samia atuma salamu za rambirambi ajali iliyoua watu 18

DODOMA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Balozi Dkt. Batilda Salha Burian kufuatia vifo vya watu 18 vilivyotokea katika ajali ya gari.

Ajali hiyo imetokea leo saa 5 asubuhi katika kata ya Uchama, tarafa ya Nyasa wilaya ya Nzega mkoani humo.Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao waliopoteza maisha ni wanaume 14 akiwemo mtoto mmoja na wanawake wanne.
 
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Oktoba 21, 2023 na Zuhura Yunus ambaye ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu.

Majeruhi ni 60 ambapo majeruhi 51 wanatibiwa Hospitali ya Wilaya ya Nzega, 19 wako Hospitali ya Rufaa ya Nkinga, 1 anatibuwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando na tisa wametibiwa na kuruhusiwa.

ACP Abwao amesema ajali hiyo imehusisha basi la kampuni ya Alfa lililokuwa likisafiri kutoka Mwanza kwenda Dar es Salaam ambalo liligongana na lori la mafuta lililokuwa likitoka Dar es Salaam kuelekea Mwanza.

Rais Samia amewapa pole majeruhi wa ajali hiyo pamoja na wafiwa wote na ameungana na familia hizo katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu wote mahali pema Peponi. Amin

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news