Rais Dkt.Samia:Serikali itaimarisha mazingira ya uchimbaji wa madini

DODOMA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewaasa wachimbaji wadogo kuachana na vitendo vya utoroshaji madini.

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse kuhusiana na jinsi wanavyowasaidia wachimbaji wadogo wa Madini katika mabanda ya Maonesho yaliyopo kwenye ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Rais Samia ametoa wito huo leo wakati akihutubia kwenye hafla ya uzinduzi wa mitambo ya uchorongaji kwa ajili ya wachimbaji wadogo pamoja na mitambo ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO).

Aidha, Rais Samia amesema wachimbaji wadogo hawana budi kuunga mkono jitihada za serikali kwa kuhakikisha kuwa wanauza madini yao katika viwanda vya ndani vya kusafisha dhahabu ili kuchochea uchumi wa viwanda.

Vile vile Rais Samia amewataka wachimbaji hao kufuata sheria, kanuni na miongozo iliyopo katika sekta ya madini ili kuhakikisha kuwa rasilimali za madini zinawanufaisha wananchi na kuchochea maendeleo ya uchumi wa nchi.

Rais Samia pia amewahakikishia wachimbaji wadogo wa madini nchini kwamba serikali itaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha mazingira ya uchimbaji pamoja na biashara ya madini ili waweze kuchangia kwenye uchumi wa taifa.

Serikali ina mpango ambao ni sehemu ya Dira ya 2030 (Vision 2030) unaoelekeza kufanya utafiti wa madini kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya “High Resolution Airborne Geophysical Survey” ifikapo mwaka 2030.

Kama hatua za mwanzo za utekelezaji wa mpango huo, mitambo mitano yenye thamani ya shilingi bilioni 2.73 imezinduliwa ambayo iko tayari kufanya kazi katika maeneo ya wachimbaji wadogo hapa nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news