Rais Dkt.Samia awataka wananchi kujielekeza kwenye fursa

SINGIDA-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi mkoani Singida kuwa na mikakati ya kutumia fursa za kiuchumi badala ya kujikita kwenye sekta moja tu ili kuongeza kasi ya maendeleo ya mkoa.
Rais Samia ametoa tamko hilo Oktoba 16,2023 wakati akihutubia wananchi katika maadhimisho
ya miaka 60 ya mkoa huo yaliyofanyika katika uwanja wa Bombadia.

Aidha, Rais Samia amewataka viongozi kuwahamasisha wananchi kupanda mazao yanayostahamili ukame pamoja na kutumia mbegu bora na za muda mfupi.

Rais Samia pia amewahimiza wananchi kulima mazao ya alizeti, dengu na ufuta ambayo hustawi katika maeneo mengi ya mkoa wa Singida pamoja na zao la korosho ambalo pia linafanya vizuri katika maeneo mengi ya mkoa huo.

Vile vile, Rais Samia ameiagiza Wizara ya Kilimo kuhakikisha miradi ya umwagiliaji inatekelezwa katika maeneo yote yaliyobainishwa kwa ajili ya ujenzi wa skimu.

Awali Rais Samia alizindua daraja la Msingi lenye urefu wa mita 100 lililopo Wilaya ya Mkalama ambalo limegharimu kiasi cha takribani shilingi bilioni 11.2.

Akihutubia wananchi wa Mkalama Rais Samia amesema Serikali itaendelea kushughulikia changamoto za kisekta zinazoikabili wilaya hiyo hususan elimu, afya na maji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news