Serikali yatoa rai kwa wanahabari kuhusu matokeo ya sensa

ARUSHA-Wanachama wa vilabu vya waandishi wa habari kutoka Kilimanjaro, Manyara na Arusha wametakiwa kutumia taaluma waliyonayo kuelezea matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika mwaka 2022 hapa nchini.
Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongela, katika mafunzo ya siku mbili jijini yanayowakutanisha wataalamu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na wanahabari.

Amesema kuwa, waandishi wa habari ni sekta muhimu katika kutoa elimu kwa jamii juu ya namna sensa ilivyo fanyika vizuri na kwa uwazi na kuelezea matokeo ya sensa hiyo kwa upana wake.

Pia, amesema lengo la Serikali ni kuona matokeo ya Sensa yanawafikia wadau wote hususani wananchi ili waweze kuyatumia katika shughuli zao binafsi.

Sambamba na kuzitumia katika kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya nchi ikiwemo kushiriki katika kupanga, kufuatilia na kutathmini shughuli za maendeleo zinazotekelezwa na Serikali .

Amesema, kama ilivyokuwa kwa wakati wa kuhamasisha wananchi kushiriki Sensa, hivi sasa ni wakati wa kuyawasilisha kwa wananchi kwa lugha rahisi na kwa weledi kupitia taaluma ya habari.

Kamisaa wa Sensa na Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Anna Makinda amesema, sensa ya mwaka 2022 imefanikiwa kwa asilimia 99.99 ambapo takwimu hizo za sensa zinakubalika na kuaminika duniani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news